You are currently viewing GRAVITY OMUTUJJU ATAJA ORODHA YA WASANII WA KIUME ANAOWAKUBALI NCHINI UGANDA, JINA LA NAVIO LAKOSEKANA

GRAVITY OMUTUJJU ATAJA ORODHA YA WASANII WA KIUME ANAOWAKUBALI NCHINI UGANDA, JINA LA NAVIO LAKOSEKANA

Rapper kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amezua gumzo kwenye mutndao ya kijamii baada ya kuachia orodha ya wasanii bora wa kiume anaowakubali kwenye kiwanda cha muziki nchini humo.

Kwenye bango ambalo ameshare kwenye mitandao yake ya kijamii kuitangaza ngoma yake mpya iitwayo Big Boys Omutujju amejitaja kama msanii bora akifutwa na Bebe Cool, Bobi Wine, Jose Chameleone, King Saha, Eddy Kenzo, Fik Fameika, Pallaso, David Lutalo, na Ziza Bafana lakini jina la Mpinzani wake kwenye muziki wa hiphop Navio limekosekana kwenye orodha hiyo.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tusimbudde” ameenda mbali zaidi na kujinasibu kuwa wasanii ambao wamekosekana kwenye list yake hiyo sio wakubwa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda na hivyo wanatakiwa kutia bidii kwenye kazi zao.

Kama ilivyo kwa orodha ya wasanii yenye utata inayotolewa na msanii Bebe Cool, list hiyo ya Gravity Omutujju imezua gumzo miongoni mwa mashabiki wa wasanii waliokosekana kwenye orodha hiyo ambapo wamepuzilia mbali list hiyo kuwa batili kwa kusema kwamba ni ya kibaguzi.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameikubali orodha hiyo ya wasanii bora wa kiume iliyotolewa na Gravity Omutujju ambapo wamemtaka rapa huyo.

Ikumbukwe Gravity Omutujju katika siku za hivi karibuni amekuwa akijiita mfalme wa  wa muziki wa Hiphop nchini Uganda, kitu ambacho wadau wa muziki nchini humo wanaamini kuwa Navio ndiye mfalme wa muziki wa hiphop kwani ndiye alianzisha utamaduni wakurap kwa lugha ya Luganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke