You are currently viewing GRAVITY OMUTUJJU ATANGAZA KUMFADHILI KING SAHA KUSAMBARATISHA UCHAGUZI WA UMA

GRAVITY OMUTUJJU ATANGAZA KUMFADHILI KING SAHA KUSAMBARATISHA UCHAGUZI WA UMA

Rapa Gravity Omutujju amejiungana na orodha ya wasanii wanaopinga upigaji kura katika chama cha wanamuziki UMA kura kufanyika kwa njia ya mtandao.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Omutujju ametaka wapiga kura kushiriki kwenye uchaguzi wa chama hicho kwa mfumo wa kawaida wa kupanga foleni kwenye vituo vya kupigia kura.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tusimbudde” ameahidi kumfadhili king saha kifedha ili aweze kusambaratisha juhudi za uongozi wa UMA kufanya uchaguzi kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo amesema ana imani kuwa King Saha atamshinda Cindy kwenye uchaguzi ujao wa chama cha UMA kwa kuwa ana wafuasi wengi ambao wanamuunga mkono.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke