You are currently viewing GRAVITY OMUTUJJU: BEBE COOL SIO RAFIKI YANGU WA KARIBU, SIMPENDI

GRAVITY OMUTUJJU: BEBE COOL SIO RAFIKI YANGU WA KARIBU, SIMPENDI

Rapa kutoka Uganda Gravity Omutujju amefunguka na kudai kuwa hataki kuwa rafiki wa msanii mwenzake Bebe Cool licha ya kufanya wimbo wa pamoja.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Omutujju amesema hana ugomvi wowote na msanii huyo ila hajawahi pata amani akiwa karibu na bebe cool kwa sababu ni mnafiki mkubwa.

Bebe Cool na Gravitty Omuttuju walifanya wimbo wa uitwao “Kerere” mwaka wa 2017 lakini hawakuweza kutoa video ya wimbo huo.

Mwaka wa 2020 kwenye moja ya mahojiano gravity omutujju alimulaumu Bebe Cool kwa kushindwa kuandaa video ya wimbo huo jambo ambalo limetafsiriwa na wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuwa huenda ndio sababu ya wawili hao kutokuwa na mahusiano mazuri.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke