Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju anafikiria kuacha kabisa kufanya muziki wa Hiphop na kuhamia kwenye muziki wa RnB..
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Hitmaker huyo wa “Enyama” amesema anabadilisha aina ya muziki wake kutokana na muziki wa Hiphop kukosa ushindani nchini Uganda.
“I am tired of rap. I want to try RnB. I have no competition in the rap game and it is now boring,” alisema Gravity Omutujju
Kauli yake imekuja mara baada ya kutamba kuwa mwanamuziki bora nchini Uganda kuliko Jose Chameleone, Bobi Wine na Bebe Cool kufuatia hatua ya kuujaza ukumbi wa Cricket Oval, Lugogo kwa mara ya nne mfululizo.