You are currently viewing GRENADE AACHIWA HURU KWA DHAMANA

GRENADE AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Grenade ameachiwa uhuru kutoka jela ikiwa ni siku chache tangu kukamatwa kwake.

Grenade alitiwa mbaroni na polisi nchini humo kwa tuhuma za kumzaba makofi aliyekuwa mpenzi wake Kilooto baada ya uhusiano wao wa kimapenzi kuingiwa na ukungu miezi kadhaa iliyopita.

Juni mosi mwaka huu Grenade alifikishwa mahakamani ambapo alikana madai ya kumpiga na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani Kilooto mbele ya Hakimu mkazi wa Kajjansi.

Hata hivyo aliachiwa huru kwa dhamana huku akionywa kutorudia kosa la kumshambulia mpenzi wake tena.

Kesi ya Grenade itasikilizwa kwa mara ya pili Juni 29 mwaka huu na kama akikutwa na hatia ya kosa hilo, huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 2 gerezani.

Utakumbuka baada ya uhusiano wa Grenade na Ex wake Kilooto kuvunjika mrembo huyo alimuanika hadharani kuwa amekuwa akimsaliti kimapenzi na kujihusisha na vitendo vya kishirikina kwa ajili ya kumshawishi azidi kumuonyesha upendo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke