Mwanamuziki kutoka Uganda Grenade amefunguka kuhusu madai ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake waliomzidi umri.
Katika mahijiano yake hivi karibuni Grenade amesema licha ya changamoto alizokutana nazo akiwa anawachumbia, hajutii kutoka kimapenzi na wanawake wazee kwa kuwa yeye ni mtu mzima ambaye anafanya maamuzi yake binafsi.
Kauli ya imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mpenzi wake Kilooto kumfungulia mashtaka mahakamani kwa madai ya kuingia kwake bila idhini ambapo kesi yake itasikilizwa Juni 28 mwaka huu.