Miaka mitatu iliyopita bosi wa Team No Sleep alimsaini msanii Grenade kwenye lebo yake na wasanii kama Sheebah na Roden Y Kabako.
Jeff Kiwa na Grenade waliingia kwenye ugomvi na wakavunja uhusiano wao baada ya msanii huyo kususia show yake mashariki mwa Uganda.
Jambo hilo lilimfanya Grenade kujiunga na lebo nyingine ya muziki iitwayo Rydim empire inayomilikiwa na Derrick Orone.
Wawili hao hawakufanikiwa kufanya kazi pamoja kama walivyoahidiana ambapo grenade alienda mbali zaidi na kuanza kufanya kazi na meneja wa lebo ya muziki aitwaye peterson.
Sasa taarifa mpya ni kuwa Jrff kiwa amemsainisha tena Grenade ndani ya lebo yake ya muziki ya Team No Sleep.
Hata hivyo Grenade amethibitisha taarifa hiyo na kusema kwamba anaamini Jeff Kiwa atamsaidia kuupeleka muziki wake kwenye kiwango kingine.