Nyota wa muziki wa injili nchini Guardian Angel ameripotiwa kufunga ndoa ya siri na mchumba wake Esther Musila baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja.
Kulingana na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii,Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri imiefanyika leo jijini Nairobi na kuhudhuriwa na wageni wasiozidi 20, ikiwemo ndugu wa pande zote mbili za familia zao.
Hata hivyo mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamiii wamefurahia kwa hatua ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao huku wengine wakiwa na mshangao kwanini ndoa hiyo imekuwa ya siri japokuwa ni jambo la kheri kwa kila mwanadamu
Uhusiano wa kimapenzi wa hao ulianza mapema mwaka jana 2021, huku Guardian Angel akithibitisha mahusiano hayo rasmi baada ya ukaribu wake na mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 51 gumzo mtandaoni ambapo wengi walishangazwa na hatua ya msanii huyo kutoka kimapenzi na mtu ambaye amemzidi umri.