Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa amekuwa akilelewa na mke wake Esther Musila.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amenyosha maelezo kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa yeye ndiye huwa anagharamia mahitaji yote ya msingi kwa mke wake kama mume.
“Hajawai kulipa bills za nyumba yangu kwa sababu mimi ndo bwana yake, mimi ndo nalipa bills zake. Na pia kama kuwekwa ni namna hiyo basi mimi sielewi. Na kama mtu anahisi hio ndo kuwekwa basi iko tu sawa. Si mimi ndo nawekwa, wewe unawashiwa nini,” Amesema.
Hitmaker huyo wa Nadeka ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kama kufurahia ndoa na kupendwa ndio imewaaminisha watu kuwa analelewa na mke wake Esther Musila, basi yupo radhi kufanya hivyo.
“Kama hivi ndo kuwekwa inaonjaacha niwekwe milele wacha niwekwe zaidi, ni tamu. Because kama nimewekwa hata sifai kupost anything ya the lady I’m purported to be with. I have never said that she is my sugar mummy secondly, I have never lived in her house, it is her who came to my house, kwa hiyo mimi ndo mzee wa hiyo nyumba.” Amesisitiza Guardian Angel.