Nyota wa muziki nchini Guardian Angel amemtambulisha rasmi msanii mpya ndani ya lebo yake ya muziki ya Seven Heaven Music.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amesema msanii huyo kwa jina la DJ Kezz kenya atakuwa chini ya lebo ya Seven Heaven Music ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki ambapo amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Deka” amesema ametumia kiasi cha shillingi milllioni 6 kutambulisha msanii huyo kwa mashabiki ikiwemo kutayarisha video za nyimbo zake tatu ambazo zitatoka karibuni.
Kwa upande wake DJ Kezz kenya ambaye ni msanii wa kwanza kujiunga na lebo ya Seven Heaven Music, ameonyesha furaha yake kujiunga na familia ya Seven Heaven Music kwa kusema kwamba mashabiki wakae mkao wa kula kupokea nyimbo zake.
Utakumbukwa kwa sasa DJ Kezz kenya anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Jipende aliyomshirikisha bosi wake Guardian Angel ambao una zaidi ya views laki moja kwenye mtandao wa youtube ndani ya siku 4 tangu iachiwe rasmi.