You are currently viewing GUARDIAN ANGEL AMVUA NGUO ANDREW KIBE KWA KUIKOSOA NDOA YAKE NA ESTHER MUSILA, AMUITA JINI SHETANI

GUARDIAN ANGEL AMVUA NGUO ANDREW KIBE KWA KUIKOSOA NDOA YAKE NA ESTHER MUSILA, AMUITA JINI SHETANI

Msanii wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel amemtolea uvivu mwanahabari mwenye utata Andrew Kibe kwa madai ya kuikosoa ndoa yake na mke wake Esther Musila.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amemtaka kibe aheshimu maamuzi yake na mke wake Esther Musila kuhalilisha ndoa kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa wao ni watu wazima ambao upendo uliwaleta pamoja licha ya utofauti wa umri wao.

“Maandiko matakatifu yanasema wakati mtu ameokoka aki-backslide, nini umu-happenia?…huwa anakuwa hatari zaidi kwani huwa anaingiliwa na shetani mara saba. Sina muda wa kupishana na shetani, vita vyetu ni vya kiroho my friend”..amesema kwenye mahojiano na Plug TV.

Hitmaker huyo wa “Nadeka” ameenda mbali na kumshauri Kibe akome kuingilia maisha yao na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye shughuli zitakazomuingizia kipato kwani anapoteza muda wake kuzungumzia jambo ambalo litamsaidia maishani.

Kauli ya Guardian Angel imekuja mara baada ya Andrew Kibe kuonekana kukejeli ndoa yake na mke wake Esther Musila kwa kusema kwamba haoni ndoa hiyo ikidumu kwani msanii huyo aliwavunjia heshima vijana wa Kenya kwa hatua kumuoa mwanamke aliyemzidi kiumri.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke