You are currently viewing GUCHI AKANUSHA KUFUNGIWA HOTELINI NAIROBI

GUCHI AKANUSHA KUFUNGIWA HOTELINI NAIROBI

Mwanamuziki wa Nigeria Guchi amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa amefungiwa kwwnye moja ya hoteli jijini Nairobi kutokana na kushindwa kulipa pesa za chakula na malezi.

Akizungumza na Nairobi Gossip Guchi amesema madai ya kufukuzwa kwenye hoteli alimokuwa anaishi kwa kusema kwamba promota ambaye alimleta Kenya anamweka vizuri huku akidokeza kuwa amehamia kwenye hoteli kubwa kutokana na wingi wa watu wanaomsimamia kimuziki.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Jeniffer amewataka mashabiki zake kupuzilia mbali madai hayo kwa kuwa promota wake ana uwezo wa kumpa kila kitu anachokihitaji.

Kauli yake imekuja mara baada ya mmoja waandaji wa onesho lake hapa Kenya kudai kuwa Promota aliyempa mwaliko amefulia kiuchumi kiasi cha kushindwa kugharamia mahitaji ya msingi ya msanii wake Guchi.

Jamaa huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa Guchi amekuwa akilala njaa lakini pia amekosa sehemu ya kulala.

Guchi anatarajiwa kutumbuiza usiku wa leo nchini Kenya kwenye tamasha lake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke