Kundi la muziki nchini Hart the Band limetangaza ujio wa album yao mpya ambayo itaingia sokoni mwaka huu.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, limetoa taarifa hiyo iliyoambatana na picha yenye ujumbe “NEW ALBUM LOADING” ikiashiria wapo kwenye maandalizi ya album mpya.
Hii inaenda kuwa album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘ iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021.