Mwanamuziki wa Bongofleva H.Baba amefunguka kuhusu madai ya kutofaidi na mirabaha ya wimbo wa Attitude aliyoshirikishwa na Harmonize.
Kuptia ukurasa wake wa Instagram H.Baba amesema ameamua kumuachia Mungu suala hilo na kwa sasa amerudi kwenye maisha yake ambayo hadhulumiwi.
“Kila chenye mwanzo kina mwisho mdogo wangu, haya yote yatakurudia tu, utadhulumika na wewe na utalalamika kama ulivyolalamika pale Airport, ila jasho langu mimi Mungu atanilipia” – Ameandika H.Baba.
H.Baba amefunguka hayo baada ya kudai kudhulumiwa jasho lake kutokana na ushiriki wake katika wimbo wa Attitude ambao alidai kuwa hakupata chochote katika pande zote mbili yaani audio na video ambapo alienda mbali na kumtaka Harmonize amlipe