You are currently viewing H. BABA AMJIA JUU HARMONIZE KISA MIRAHABA YA WIMBO WA ATTITUDE

H. BABA AMJIA JUU HARMONIZE KISA MIRAHABA YA WIMBO WA ATTITUDE

Mwanamuziki wa bongofleva, H. Baba ameibuka kudai haki yake kutoka kwa Harmonize ambaye wamewahi kufanya nae kazi ya ushirikiano kupitia wimbo wa “Attitude” ambao ulitoka Aprili 23, mwaka jana akiwemo pia gwiji kutoka DR Congo, Awilo Longomba.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, H. Baba amedai kudhulumiwa jasho lake kutokana na ushiriki wake katika wimbo huo kwa kutoambulia chochote katika pande zote mbili yaani audio na video ambapo amemsihi kwamba Harmonize amlipe.

“Nakuheshimu sana, usidhulumu jasho langu mdogo wangu” inasomeka sehemu ya ujumbe wa H.Baba aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wimbo “Attitude” ni moja kati nyimbo kutoka kwa Harmonize iliyopata mafanikio makubwa, hadi sasa video ya wimbo huo ina views Milioni 15 katika mtandao wa youtube huku Boomplay ikiwa na streams Milioni 2.1

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke