Mwanamuziki wa Bongofleva H.Baba ameweka wazi kulipwa kiasi kikubwa cha fedha na Diamond Platnumz kuwa balozi wa kampuni yake ya michezo ya kubashiri ya wasafi bet.
Baba, ametumia Instagram page yake kutoa pongezi na shukrani kwa msanii huyo na uongozi mzima wa WCB, ambao awali alionekana kuwarushia maneno makali mtandaoni kwa ajili ya kumsapoti mwanamuziki Harmonize.
Katika hatua nyinngine H. Baba ameweka wazi kuhusu kumuandalia Diamond Platnumz tuzo yake binafsi kama ambavyo amekuwa akifanya kwa Harmonize.
H.Baba ametangaza kuwa shabiki rasmi wa WCB Wasafi huku akiwaomba radhi mashabiki wa lebo hiyo.