Mwanamuziki wa Bongofleva, H. Baba kwa sasa anam-follow Diamond Platnumz pekee kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao una followers zaidi ya laki 6.
Juzi kati H. Baba alimpongeza Diamond kwa kutumbuiza kwenye show maalumu iliyoandaliwa na waandaaji wa tuzo za Grammy, Recording Academy iitawayo Global Spin ambayo ina lengo la kuuibua na kuutangaza zaidi muziki wa Afro Beat, Pop na Latin Music.
Hatua hiyo iliwashangaza wengi kwani kwa miaka ya hivi karibuni H. Baba alikuwa karibu sana na Harmonize hadi kushirikiana kwenye wimbo, uitwao Attitude ambao Awilo Longomba kutoka DRC Congo naye alishirikishwa.
Kwa inavyoonekana sasa uhusiano kati ya H. Baba na Harmonoze umeingia na ukungu baada ya kuamua kumu-unfollow Instagram na kum-follow Diamond pamoja na kuupigia debe muziki wake.