Mshindi wa tuzo ya Grammy, mwimbaji H.E.R, ameishitaki lebo yake ya muda mrefu ya MBK Entertainment, ambayo inamilikiwa na Jeff Robinson kwa ukiukaji wa kanuni ya biashara na taaluma.
H.E.R ambaye jina lake halisi ni Gabriella Sarmiento Wilson , amekuwa chini ya lebo ya MBK kwa kipindi cha zaidi ya miaka 11, alisainishwa na lebo hiyo akiwa na miaka 14.
Kesi yake iliwasilishwa wiki iliyopita Juni 16, katika Mahakama Kuu ya Jimbo la California, huko Los Angeles nchini Marekani.