You are currently viewing HALIMA NAMAKULA ACHOSHWA NA UPWEKE, ATAKA MWANAUME WA KUMLIWAZA

HALIMA NAMAKULA ACHOSHWA NA UPWEKE, ATAKA MWANAUME WA KUMLIWAZA

Mwanamuziki mkongwe kutoka uganda Halima Namakula amechoshwa na maisha ya kuwa mpweke kwa takriban miongo mitatu.

Katika mahojiano yake ya hivi karibu mwanamama huyo ambaye ana umri wa miaka 62 amewapa changamoto watoto wake kumtafutia mume wa kumpenda.

Halima Namakula amesema kuwa anataka mwanamume ambaye atakidhi matamanio yake ya kimwili na awe na umri kati ya miaka 55 na 60.

“Ndio, ninatafuta, Watu wamekuwa wakiniambia nianze kuchumbiana tena na nadhani ni wakati sahihi. Nataka watoto wangu wanipatie mwanamume ambaye ni mdogo kwangu kwa miaka mitatu, mwenye nguvu, na mwenye pesa nyingi kwa sababu sitoi pesa, mimi ni wa kizamani,” alisema kwenye mahojiano.

Utakumbuka baba wa watoto wake alifariki mwaka wa 1994 na tangu kipindi hicho amekuwa akiwalea watoto wake bila usaidizi wa mtu yeyote.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke