Mrembo na msanii wa Tanzania Hamisa Mobetto amekana madai kwamba yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Rapa wa Marekani Rick Ross.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya NTV, Msanii huyo ambaye pia ni mfanyabishara amethibitisha kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa rapa huyo wa Marekani.
Wawili hao wamekuwa wakihusishwa kuwa ni couple mara baada ya Novemba 25, mwaka wa 2021 kuonekana wakiwa Dubai wakila bata pamoja. Kubwa zaidi walionekana wakicheza muziki kwenye moja ya kumbi za starehe kwa kukumbatiana kimahaba.