Msanii wa Bongofleva Hamisa Mobeto ameachia rasmi EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
EP hiyo inakwenda kwa jina la Yours Truly ina jumla ya nyimbo 4 na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Otile Brown na Korede Bello.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Hamisa Mobetto ameshare artwork pamoja na Tracklist ya EP hiyo ambayo ina nyimbo kama Wewe, Want, Murua, Yanini na Pop It.
Yours Truly ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Hamisa Mobetto tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay.