You are currently viewing HAMISA MOBETTO AKANUSHA KUMFICHA MPENZI KWA HOFU YA KUPOKONYWA

HAMISA MOBETTO AKANUSHA KUMFICHA MPENZI KWA HOFU YA KUPOKONYWA

Mwimbaji na Mwanamitindo maarufu Tanzania, Hamisa Mobetto amekanusha madai kuwa amekuwa akimficha mpenzi wake wa sasa kwa kuhofia kupokonywa.

Akizungumza na Wanahabari siku ya jana, Mobetto alieleza kuwa kwa kawaida huwa hathamini kuyaanika mahusiano yake hadharani.

“Mimi naamini kama kitu ni chako na Mungu amepanga, basi kitakufikia na hakitakuwa cha kuibiwa. Siamini kama mwanaume anaweza kuibiwa” amesema.

“Sio kama namficha, mimi na yeye tuko vizuri katika mapenzi yetu. Tunakula, tunatembea pamoja, yaani tuko vizuri,” alisema Hamisa.

Pia alidai kuwa sio sawa kwake kuendelea kuwatambulisha wapenzi wapya kila wanapokuja katika maisha yake.

“Tukifika mbele huko kama Mwenyezi Mungu alimuandikia kuwa mume wangu basi huenda watu wataanza kumjua. Lakini sasa hivi kama tukiachana? nikipata mwingine tena nimtambulishe,” alisema.

Aidha, alibainisha kuwa kuweka mahusiano hadharani mara nyingi huwafanya watu waache kujizingatia na badala yake kuzingatia penzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke