Baada ya kuzawadiwa Range Rover na mpenzi wake, Mwanamitindo na Msanii wa Bongofleva, Hamisa Mobetto ameweka wazi kiu yake ya kununua private Jet.
Hamisa ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alikuwa anashukuru kwa kupata gari hilo alilokabidhiwa wikiendi iliyopita.
“Mungu hakupi unachotaka, anakupa unachostahili,” alisema Hamisa katika ujumbe wake.
Endapo Hamisa akifanikisha hilo, ataungana na wasanii wa Afrika wenye Private Jet kama Davido, Cassper Nyoves, P Square, DJ Cuppy, Wizkid na wengineo.