Mwimbaji wa Bongofleva, Hamisa Mobetto amethibitisha kuachia Extended Playlist (EP) yake mpya wiki hii.
Hamisa amebainisha hayo akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitangaza kupata dili nono la ubalozi wa Kampuni ya “House of beauty”
“Wiki ijayo natoa EP yangu, itakuwa ni ya kwanza tangia nimeanza safari yangu ya muziki, tulikuwa tunabishana kati ya kutoa albamu au tutoe EP, kwa hiyo naona jambo limekimbilia kwenye EP” amesema Hamisa.
Mbali na muziki, milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwa mwanamitindo huyo kwani ukiachilia mbali kuwa balozi wa bidhaa za urembo pia ni balozi wa kinywaji cha kishua cha Belaire.