Msanii wa Bongofleva Hanstone ameibuka na madai ya kwamba Diamond Platnumz ameiba wimbo wake kwenye kazi yake mpya “CHITAKI” ambayo ameidokeza kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia insta story yake, Hanstone ameanika wazi hilo kwa kuweka kipande cha wimbo wake uitwao “NATETEMEKA” ambapo kwenye file inaonesha aliufanya mwaka 2019.
Utakumbuka Hanstone na Diamond walikuwa na ukaribu ambapo Hanstone alikuwa anatajwa kuwa angesainishwa na lebo ya WCB lakini baada ya kutokea utofauti wa pande zote mbili dili hilo lilitajwa halikuweza kukamilika.