You are currently viewing HAPPY C AKANUSHA TUHUMA ZA KUIBA WIMBO WA HESHIMA

HAPPY C AKANUSHA TUHUMA ZA KUIBA WIMBO WA HESHIMA

Msanii kutoka 001 Music Happy C amekanusha madai ya kuiba idea ya wimbo wake mpya uitwao “Heshima” kutoka kwa Atumik wa leo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook amemtaka Atumik akome kueneza taarifa za uongo kwamba alimuibia wimbo wa Heshima huku akimtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutangaza kazi zake za muziki badala ya kutengeneza mitukio ili azungumziwe na vyombo vya habari.

Hata hivyo amesema anamheshimu Atumik kama mmoja wa mashabiki zake huku akiwataka wakenya waendelee kusapoti wimbo wake wa Heshima kwenye digital platflorms mbali mbali za muziki.

Kauli ya Happy C imekuja mara baada Atumik wa leo kumtaka msanii huyo amlipe fidia kwa kuiiba ubunifu wake na kuutumia kwenye wimbo wake mpya Heshima  la sivyo atamchukulia hatua kali za kisheria.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke