Mkali wa muziki nchini Happy Chondo maarufu kama Happy C kutoka lebo ya 001 Music amemtolea uvivu staa wa muziki nchini Willy Paul kwa madai ya kukosa ubunifu kwenye uandishi wa nyimbo zake.
Happy C ametoa kauli hiyo kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram mara baada ya Willy Paul kuachia wimbo wake mpya uitwao “Ogopa Wasanii” ambao kwa mujibu wake amekopi idea ya msanii wa Bongofleva Diamond Platinumz.
Kulingana na Happy C bosi huyo wa Saldido International anajishusha kwenye suala la uandishi wa nyimbo zake ikizingatiwa kuwa kuna wasanii wadogo na hodari ambao wana uwezo wa kuandika nyimbo zenye maudhui ya kumuelisha jamii.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha “Mariana” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba yupo tayari kumuandikia willy paul nyimbo kama ataendelea kutoa nyimbo ambazo hazina mashiko.