Baada ya mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize kuwafuta urafiki watu wote ambao alikuwa ame-wafollow katika mtandao wake wa Instagram hatimaye msanii huyo ameanza zoezi la kuwa follow back tena mashabiki na watu waliowahi kumfollow.
Ukitembelea ukurasa wa Instagram wa Harmonize utagundua ameongeza idadi ya (Following) kutoka 1 mpaka 283.
Utakumbuka mwishoni mwa mwaka wa 2021 mwanamuziki huyo ambaye ni Boss wa Konde Gang aliweza ku Un-follow mashabiki na watu wote walio mfollow na kumfollow mpenzi wake Briana.
Kulingana na mahojiano aliyoyafanya mwishoni mwa mwaka 2021 na kipindi cha XXL’ Harmonize alieleza kuwa aliamua kufanya hivyo ili kupata mapumziko na mpenzi wake.