You are currently viewing HARMONIZE AFICHUA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA MIWA

HARMONIZE AFICHUA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA MIWA

Huenda msanii wa Bongofleva Harmonize ameamua kuwekeza katika kilimo cha miwa.

Hii ni baada ya kushare video clip akiwa katika shamba la miwa na kudai ni mara ya kwanza kufika kwenye shamba hilo.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Harmonize ametoa changamoto kwa vijana kuwekeza katika aina hiyo ya kilimo kama njia ya kujikwamua kiuchumi.

“Kuna Maisha Baada Akicheza Pesa Zako Zote Club” Huku Akiwa Katika Shamba La Miwa”. Ameandika kwenye caption ya video clip yake.

Hata hivyo inatajwa kuwepo na uwezekano wa msanii huyo kutoka Konde Gang kuwa amelamba dili lingine la ubalozi katika kampuni moja ya Sukari nchini Tanzania.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke