You are currently viewing Harmonize afunguka juu ya maendeleo ya album yake mpya “Boss Lady”

Harmonize afunguka juu ya maendeleo ya album yake mpya “Boss Lady”

Msanii kutokea Konde Music, Harmonize amesema ni nyimbo nne tu ndio zimesalia ili aweze kutoa albamu kwa ajili ya mchumba wake, Kajala.

Hata hivyo, Harmonize amesema tayari kuna nyimbo kama nane zimetoka ambazo ni Deka, Nitaubeba, Mtaje, You, Utanikumbuka, Wote, Vibaya na Miss Bantu.

Albamu hiyo Harmonize ameiipa jina la ‘The Bosslady’ na anafanya hivyo kuonyesha ni kiasi gani anampenda Kajala ambaye amemteua kuwa Meneja wake na Konde Music Worldwide kwa ujumla.

Albamu hiyo itakuwa na nyimbo 12 na inatarajiwa kutoka Desemba mwaka huu ikiwa ni albamu ya nne kwa Harmonize baada ya Afro East, High School na Made For Us.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke