You are currently viewing HARMONIZE AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUMUIMBIA BAKHRESA

HARMONIZE AFUNGUKA SABABU KUBWA YA KUMUIMBIA BAKHRESA

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize kwa mara ya kwanza ametoa ufafanuzi juu wa wimbo wake mpya wa Bakhresa’ ambao umezua gumzo mtandaoni.

Kupitia ujumbe mrefu aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema sababu kubwa iliyompelekea kuimba wimbo huo ni kutoa hamasa kwa watu wasio na kipato kizuri katika jamii kupata nguvu ya kutafuta zaidi kwenye shughuli zao.

“MY MUSIC 🎶 IS MORE ABOUT LIFE & PEOPLE Binafsi Nitafarijika Zaidi Kuona Watu Wakibadirisha Mwenendo Wa Maisha Kupitia Wimbo Huu ..!!!! Nitafarijika Sana Kumuona Kijana Mwenzangu Yeyote Mtaani Mwenye Kipato Kidogo Akiutumia Huu Wimbo Kama WEK UP CALL Na Kumtazama BAKHRESA Kama Mfano Wa Wazi …!!! Na Kuanza Zikimbilia Ndoto Kubwa Zaidi Nitafarijika Kuona Hakuna Kudharauliana Tunaishi Kwa Heshima Na Usawa Bila Kujali Hapa INTAGRAM Una Followers Wangapi ..!!! Maisha Ya BAKHRESA Ni Mfano Bora Wakuigwa Ingawa Sio Lazima Kila Tajiri Aishi Kama Anavyoishi BAKHRESA ..!!!” ameandika Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” ameendelea kwa kusema “Nimalize Kwakusema MZEE BAKHRESA KUSIKIA WIMBO HUU Haitokuwa Ni Jambo La Ajabu Kwake Kwasababu Niliyo Ya Sema Yote ANAYAFANYA mafanikio Niliyo Yataja Yote Anayo Na Bila Shaka Haya Ni Machache tuu …!!! Kama Angetaka Kuimbwa Basi Angemlipa Hata (DRAKE) Maaana Uwezo Huwo Bila Shaka Anao Binafsi Sina Haja Kabisa Ya Mzee BAKHRESA kuusikia Wimbo Huu Maaana Ningetaka Hivyo Basi Ningefanya Utaratibu Wa Kuitafuta Familia Yake Ndugu Jamaa Na Marafiki ILI WIMBO UMFIKIE ASIKILIZE KAMA LENGO LILIKUWA NI KUMSIFIA ..!!!”

Harmonize amemalizia kwa kusema “KIFUPI SINA URAFIKI AU UKARIBU WOWOTE NA NDUGU WA MZEE (BAKHRESA) LENGO LANGU KUBWA …!!! HUU WIMBO UKUFIKIE WEWE MASKINI MWENZANGU ULIENYANYASIKA NA MASKINI WENZAKO AMBAO WANAKUZIDI KIPATO KIDOGO TUUU UPATE NGUVU 💪🏼 NA UAMKE TENA ..!!! 💪🏼💪🏼 WIMBO HUU UKUFIKIE WEWE MWENYE NDOTO NDOGO UACHANE NAYO UTAFUTE KUBWA ZAIDII ….!!!! MWISHO WE THANK GOD FOR THE LIFE OF BIG BOSS (BAKHRESA )
PIA WALE MNAOSEMA NIMEFANYA TANGAZO LA BURE …!!! NI WAKATI WAKUWAKUMBUSHA MATAJIRI WENGINE WAYAFANYE MEMA YA KUMPENDEZA MUNGU & BINADAMU ILI WAPATE MATANGAZO YA BURE KAMA HAYA …..!!!! PERIOD NO ONE LIKE BAKHRESA Link in bio”

Kauli ya mtu mzima Harmonize imekuja mara baada ya walimwengu kwwnye mitandao ya kijamii kumbeza kuwa ameishusha Brand au chapa yake ya muziki kwa kuachia wimbo wa bure kutangaza biashara na kampuni zinazomilikiwa na tajiri huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Azam ya nchini Tanzania.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke