Mwanamuziki na Rais wa lebo ya Konde Music Worldwide Harmonize ametangaza kuingia kwenye fani ya uigizaji muda wowote kutoka sasa.
Harmonize ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake Women alichoshirikiana na Otile Brown ameweka wazi hilo kupitia InstaStory yake ambapo ameandika kuwa filamu hiyo kwa mara ya kwanza itaoneshwa kupitia mtandao wa Ceek.
Harmonize ameandika “Nimechoka kusubiri filamu yangu ya kwanza. Itakuwa kali sana, tukutane Ceek hivi karibuni jisajili sasa”
Kampuni ya Ceek ni kampuni ambayo inajihusisha na maswala ya burudani kama kurusha matukio ya mubashara mtandaoni, kuandaa matamasha, na kutengeneza headphones.