Mkali wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameitawala Twitter kwa upande wa Tanzania, staa huyo wa muziki wa bongo fleva ameusimamisha mtandao huo wa Kijamii kwa Jina lake kukaa namba 1 kwenye orodha ya ‘Topics’ ambazo zinazungumzwa zaidi kwenye mtandao huo nchini Tanzania.
Hadi sasa mtandao huo unaonesha jina la harmonize limeongelewa kwenye zaidi ya Tweets 5,893 ikiwa ni masaa 24 tu tangu afunguke mazito kuhusu menejimenti yake ya zamani (WCB) pamoja na msanii diamond platnumz