Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameendelea kushusha sifa kwa mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy kwa hatua kubwa anazopiga katika muziki wake kimataifa na kusema kuwa wapambanaji pekee ndio wanaweza kumuelewa.
Kupitia instastory yake ameshare ujumbe akisisitiza kuwa Burna Boy ndiye msanii namba moja kwa sasa Afrika huku akitaja baadhi ya matukio aliyojifunza kutoka kwa Staa huyo kipindi yupo Lagos, Nigeria na kusema kuwa hakuwahi kumsikia Burna Boy akimzungumzia mtu vibaya lakini pia akijisifia juu ya mafanikio yake na tuzo alizonazo .
Mbali na hayo, Harmonize amesema kila mtu ana uhuru wa kumtaja Staa anayehisi ni namba moja kwa sasa barani Afrika lakini wasisahau kuwa yeye ndio anayefuata baada ya Burna Boy.
Harmonize na Burna Boy tayari wameshafanya nyimbo mbili za pamoja ambazo ni Kainama inayopatikana kwenye Afro Bongo EP ya mwaka wa 2018 pamoja na Shake your body inayopatikana kwenye album ya Afro East ya mwaka wa 2018.