Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize amekana na kukataa madai ya uwepo wa video ya wimbo wake uitwao Mtaje” ambao aliuimba mahususi kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Frida Kajala, kufuatia kusambaa kwa bango linalo onesha picha yake na mrembo huyo.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram Harmonize ameendelea kushare mfululizo wa post zinazo eleza kumkumbuka mpenzi wake huyo wa zamani huku akisisitiza kwamba hafanyi hivyo kwa ajili ya promotion ya wimbo wake wa Mtaje’.
Mbali na hayo hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amejitapa kuwa mwanamuziki alie sikilizwa zaidi Afrika Mashariki katika mtandao wa Spotify baada ya kufikisha jumla ya streams laki 8 katika mtandao huo huku akidai kwa sasa anaweza tabasamu kufuatia hilo.