You are currently viewing HARMONIZE AMPA ZA USO DIAMOND PLATINUMZ, ADAI ANAMFANYIA FIGISU APOTEE KIMUZIKI

HARMONIZE AMPA ZA USO DIAMOND PLATINUMZ, ADAI ANAMFANYIA FIGISU APOTEE KIMUZIKI

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ambaye ni mmiliki wa lebo ya muziki ya Konde Gang, amefunguka mengi kuhusu sakata la kutokuwa na maelewano na aliyekuwa boss wake Diamond Platnumz ,mara baada ya kutua nchini Tanzania akitokea nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki.

Katika sakata hilo Harmonize ameeleza kuwa ugomvi wake ulianza baada ya yeye kuonekana anafanya vizuri kumzidi boss wake ambaye ni Diamond Platinumz na tangu aondoke WCB bosi wake huyo wa zamani amekuwa akifanyia figisu aonekana mbaya kwa jamii lakini pia asifanikiwe kimuziki.

Harmonize amesema kipindi yupo chini ya lebo WCB diamond alikuwa anamkata asimilia 60 ya mapato yake ya muziki huku akimlipa asilimia 40 ambayo anasema alitumia kutanua wigo wa muziki wake kwa kuwashirikisha wasanii wa mataifa mengine jambo ambalo anadai halikumfurahisha diamond kwa kuwa alikuwa anahisi anamshinda kimuziki.

Hitmaker huyo wa Teacher anasema kuna kipindi alikuwa anakatazwa kutembelewa na baba yake mzazi kwa kuwa alikuwa anakuja kumroga Diamond Platnumz jambo ambalo lilimkosesha amani hadi ikampelekea kuvunja mkataba wake na WCB.

Harmonize amesema mchakato wa kujiondoa WCB ilikuwa na changamoto nyingi ila anamshukuru aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli kwa kumkingia kifua hadi akapewa barua ya kuvunja mkataba wake na WCB, kwani Diamond Platinumz alikuwa amedinda kumpa barua hiyo kwa kumlimbikizia gharama zisizo kuwa na msingi ilmradi tu asambaratishe harakati zake za kuwa msanii wa kujitegemea.

Bosi huyo wa Konde Gang amesema kuwa anazungumza vizuri na mama watoto wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna, Zari the Boss Lady na Hamisa Mobetto lakini hajawahi kupiga nao hata picha kwa kuwa atakuwa anamvunjia heshima Diamond Platnumz.

Hata hivyo ameongea kwa masikitiko makubwa sana akimlaumu aliyekuwa boss wake Diamond Platnumz kuwa anawalipa Baba levo na Juma Lokole ili wamtukane mtandaoni huku akisema kama bosi wake huyo wa zamani angekuwa anataka heshima anayoidai kwake angewakataza baba levo na juma lokole kumzungumzia vibaya kwenye mitandao ya kijamii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke