You are currently viewing HARMONIZE AMTAMBULISHA KWA MARA YA KWANZA MPENZI WAKE MPYA

HARMONIZE AMTAMBULISHA KWA MARA YA KWANZA MPENZI WAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva Harmonize ameingia kwenye penzi zito na mrembo kutoka Australia ambaye anafahamika kwa jina la Briana.

Mrembo huyo mwenye umri wa kati ya miaka 22 na 25, anatajwa kuwa ni modo na balozi wa kutangaza mavazi huku mambo mengine akiyaweka kuwa ni binafsi.

Tetesi za Harmonize  kuwa kwenye penzi na mrembo huyo zilianza kuvujishwa na Harmonize mwenyewe kupitia ukurasa wake wa Instagram Novemba 13 baada ya kuposti picha ya mkono wa mrembo huyo akiwa ameshika picha yao wakiwa pamoja huku akiambatanisha na maneno yanayosomeka “What a Memory”.

Hakuishia hapo, Boss huyo wa Konde Gang aliposti pia ujumbe unaosomeka, “Finally I have the woman of my life”

Katika kutilia mkazo juu ya penzi lake hilo jipya, Novemba 15, harmonize ameweka wazi mpango wa kuwa un-follow watu wote na kum-follow mwanamke huyo pekee anayempenda. Hata hivyo amebainisha kuwa anawapenda watu wote na kuwaheshimu licha ya kuwa un-follow.

Ikumbukwe Briana kutoka Australia anakuwa mwanamke wa pili mwenye asili ya kizungu kuwa kwenye mahusiano na harmonize, kabla ya hapo Harmonize alikuwa kwenye ndoa na Sarah Michelloti kutoka Italia kabla ya ndoa yao kuvunjika.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke