You are currently viewing HARMONIZE AMVISHA PETE YA UCHUMBA KAJALA MASANJA

HARMONIZE AMVISHA PETE YA UCHUMBA KAJALA MASANJA

Msanii wa Bongofleva Harmonize amemvisha pete ya uchumba Mwigizaji Kajala Masanja ikiwa ni siku chache toka wawili hao warudiane baada ya penzi lao kuvunjika kipindi cha nyuma.

Tukio hilo limefanyika Jumamosi Juni 25,mwaka 2022  katika hoteli ya Serena huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang.

Wakati wa tukio hili Harmonize amekiri kwamba Kajala ni Mwanamke bora kwake na kuna wakati Kajala alimpa hifadhi kwenye nyumba yake wakati Harmonize akiwa hana nyumba.

Harmonize na Kajala wamechumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu walipotengana baada ya mwanamuziki huyo kumfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke