You are currently viewing Harmonize aomba radhi kwa kuhamasisha matumizi ya bangi

Harmonize aomba radhi kwa kuhamasisha matumizi ya bangi

Baada ya mamlaka ya kupambana na Dawa za kulevya nchini kuonya wasanii wanaotunga nyimbo zinazo hamasisha matumizi ya dawa za kulevya na baadae mwanamuziki Harmonize kuonekana BASATA akipewa maelekezo kuhusu sanaa yake, hatimae Uongozi wa Konde Gang umeomba radhi.

Kupitia mitandao yao ya kijamii uongozi wa Konde Music Worldwide umeomba radhi kufuatia wimbo wa msanii wao Harmonize unaoitwa “Weed Language” wenye mahudhui yanayo zungumzia kuhusu bangi

“Wimbo huu ulilenga kupanua na kukuza muziki wetu nje ya mipaka ya nchi yetu.

“Lakini tafsiri ya maudhui ya wimbo huo yanakiuka maadili, utamaduni, mila na desturi pamoja na miongozo ya mamlaka za serikali nchini.

“Kutokana na kadhia iliyosababishwa na maudhui ya wimbo huo tunaomba radhi na tunaahidi kuuondoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.

“Pia tunaahidi kuboresha nyimbo zetu ili ziendane na utamaduni wetu pamoja na miongozo ya mamlaka ya serikali”

Hata hivyo mpaka sasa wimbo wa ‘Weed Language umeondolewa katika mtandao wa Youtube lakini bado unapatikana katika ukurasa wa instagram wa Kondegang.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke