You are currently viewing HARMONIZE AONDOA MAJINA YA WASANII JUX NA DARASSA KWENYE BANGO LA TAMASHA LAKE  “AFRO EAST CARNIVAL”

HARMONIZE AONDOA MAJINA YA WASANII JUX NA DARASSA KWENYE BANGO LA TAMASHA LAKE “AFRO EAST CARNIVAL”

Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ameyaondoa majina ya wasanii Jux na Darassa kwenye bango lenye orodha ya wasanii ambao wametajwa kutumbuiza kwenye tamasha la Afro East Carnival.

Kwenye bango jipya ambalo Hitmaker huyo wa “Outside” ameliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, majina ya wakali hao yameondolewa kufuatia malalamiko yao kwamba hawakuwa na taarifa yoyote au makubaliano na menejimenti ya Harmonize.

Tamasha la Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam Machi 5, mwaka wa 2022 na litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki.

Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kupanga kufanyika kwa tamasha kubwa la muziki nchini tanzania, August 4 mwaka wa 2020 aliitambulisha rasmi Harmo night Carnival ambayo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huo kwa siku tatu mfululizo.

Hata hivyo tamasha hilo halikufanyika kwa sababu ambazo hadi leo hazijawekwa wazi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke