Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize bado anaendelea kuzitukuza Tuzo zake Tatu ambazo alishinda kwenye tuzo za Tanzania Music Awards mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema haitaji Tuzo za nje kama Grammy, BET na zote za Kimataifa kama hatofanikiwa kushinda za Tanzania kwani kizuri huanzia nyumbani.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” anaonekana ana mipango mikubwa na Tuzo za Tanzania kwani amewasisitizia mashabiki zake kumuombea kichwa chake kikae sawa hadi mwakani utakapofanyika msimu mwingine.
“It was a Dream..!!! Happy to See Tanzania Music Awards Back ..!!! 🙌 I don’t Need Grammy & BET & And All International Awards if I Don’t Wen This ..!!! START FROM HOME #TMA2021 TRIPPLE BEST 🏆🏆🏆 Niombeeni Tuu Kichwa Kikae Sawa Then Tukutane #TMA2022 🤞@amherman_ 🎬 PLEASE…!!!! PLEASE …!!!! PLEASE …!!! DO NOT SLIDE 🔞,” Ameandika Instagram.