Msanii nyota wa Bongofleva Harmonize ametangaza rasmi bidhaa yake ya Sigara iitwayo “Tembo Cigarette”.
Kupitia Instagram yake Harmonize ameomba wadau kuwekeza pesa lakini pia washirika wa Kibiashara wajitokeze kwa ajili ya kuisukuma biashara hiyo.
Ikumbukwe boss huyo wa Konde Gang tarehe 5 mwezi huu kupitia insta story yake aliweka wazi kwa mara ya kwanza kuwa amepata wazo la kuanzisha chapa (brand) yake mwenyewe ya Sigara na yuko tayari kuwekeza katika biashara hiyo.