CEO wa record label ya KondeGang Harmonize ametangaza rasmi ujio wa remix ya wimbo wa dini uitwao “Omoyo” kutoka kwa mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Tanzania Jane Misso
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kumchana mwimbaji wa nyimbo za injili Goodluck Gozbert kwa tafsiri ya kutomzungumzia vizuri juu ya matamanio yake ya kufanya muziki huo wa injili.
Mbali na hayo Harmonize ambaye ni muumini wa dini ya kiislam ameeleza kuwa yeye ni bado ni muumini wa dini ya kiislamu na ataendelea kuwa na upendo kwa watu wa dini zote bila kujali utofauti wa imani zao.