Baada ya kuachia album yake mpya “High School” bila kuwashirikisha wasanii wa Kenya, Staa wa muziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza ujio wa EP yake mpya iitwayo “Gengefleva”.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Harmonize amesema Ep hiyo itakuwa na jumla ya mikwaju 5 ya moto ambapo atawashirikisha wasanii wa kenya wenye vipaji bila kuangalia ukubwa wa msanii.
Hitmaker huyo wa “Teacher” amedokeza mpango wa kufanya ziara ya kimuziki kwenye miji kumi za kenya ambapo amewapa nafasi mashabiki zake wakenya kupendekeza majina ya miji ambayo wangependa afanye tamasha lake la muziki.
Kauli ya Harmonize imekuja mara baada ya kutangazwa kuwa moja kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Mseto Festival ambalo litaanza Disemba 12 mwaka huu katika kaunti ya Kakamega na kisha baadae kufanyika kwenye kaunti zingine za humu nchini