You are currently viewing HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA AFRO EAST CARNIVAL KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA AFRO EAST CARNIVAL KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Mwanamuziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza ziara yake ya muziki iitwayo “Afro East Carnival” ambayo itaanza baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa waumini wa dini ya kiisilamu.

Boss huyo wa Konde Gang ametoa ratiba ya tamasha la Afro East Carnival kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema atafungua ziara hiyo nchini Kenya kwa kuanza na show jijini Nairobi tarehe 30 mwezi Aprili kisha ataelekea Mombasa tarehe Mosi mwezi Mei.

Mei 15, atakuwa jijini Bujumbura nchini Burundi, huku Mei 29 akirejesha burudani jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea Uganda Juni 06 mwaka huu.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Outside” amesema Akitoka Uganda, ataelekea jijini Kigali nchini Rwanda tarehe 18 mwezi Juni ambapo atakamilishia ziara hiyo jijini London nchini Uingereza ya Afrika Mashariki Tarehe 30 mwezi Juni.

Hata hivyo amesema Tamasha hilo ambalo lilipata mapokezi makubwa jijini Dar es salaam mapema mwezi huu limedhaminiwa na jukwaa la mtandaoni la Ceek.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke