You are currently viewing HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA “AFRO EAST CARNIVAL”

HARMONIZE ATANGAZA UJIO WA TAMASHA LA “AFRO EAST CARNIVAL”

Mwanamuziki wa bongofleva Harmonize ameitangaza rasmi Machi 5, mwaka wa 2022 kuwa tarehe rasmi ambayo tamasha lake ‘Afro East Carnival’ litafanyika Jijini Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wake, tamasha hilo litawakutanisha kwenye steji moja nyota wakubwa kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki.

Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kupanga kufanyika kwa tamasha kubwa la muziki nchini tanzania, August 4 mwaka wa 2020 aliitambulisha rasmi Harmo night Carnival ambayo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huo kwa siku tatu mfululizo.

Hata hivyo tamasha hilo halikufanyika kwa sababu ambazo hadi leo hazijawekwa wazi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke