Nyota wa muziki wa Bongofleva Harmonize ametangaza ujio wa tamasha lake liitwalo Afro East Carnival ambapo ameweka wazi kwamba litafanyika Februari 14 mwaka 2022.
Kwenye andiko lake kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram, Konde Boy amesema tamasha hilo litawajumuisha wakali wa muziki Afrika Mashariki kwenye uwanja mmoja Jijini Dar Es Salaam.
Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kupanga kufanyika kwa tamasha kubwa la muziki nchini, August 4 mwaka wa 2020 aliitambulisha rasmi Harmo night Carnival ambayo ilipangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana kwa siku tatu mfululizo.
Hata hivyo tamasha hilo halikufanyika kwa sababu ambazo hadi leo hazijawekwa wazi.