Msanii wa Bongofleva, Harmonize ametangaza tour barani Ulaya kwa ajili ya albamu yake ya pili, High School.
Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide amethibitisha ujio wa ziara hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema itaanza Julai 2 hadi Agosti 6 mwaka huu.
Harmonize ambaye anafanya vizuri na ngoma yake “Bakhresa” atapita kwenye mataifa kama Ufaransa, Ujerumani, Hungary, Denmark, Sweden na Finland.
Ujio wa tour hiyo yenye show tisa inakuja wiki chache tangu Harmonize aitangaze ziara yake ya Afrika Mashariki ya “Afro East Carnival” ambayo itaanza baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa waumini wa dini ya Kiislamu.