You are currently viewing HARMONIZE AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA MKATABA WA COUNTRY BOY KUMALIZIKA KONDE MUSIC WORLDWIDE

HARMONIZE AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA MKATABA WA COUNTRY BOY KUMALIZIKA KONDE MUSIC WORLDWIDE

Siku chache baada ya Lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide kutangaza kumalizika kwa mkataba baina yao na msanii Country Boy, mmiliki wa lebol hiyo Harmonize ametoa neno.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, Harmonize amemshukuru Country Boy kwa uwepo wake ndani ya Konde Music Worldwide katika kipindi cha miaka miwili, lakini pia amemtakia kila la kheri na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano kwenye kazi zake.

Uongozi wa lebo ya Konde Music Worldwide ukiongozwa na harmonize  walifanya party maalumu ya kumuaga msanii Country Boy ambaye alimaliza mkataba na lebo hiyo January 08, mwaka wa 2022.

Party hiyo ilifanyika nyumbani kwa Harmonize na kuudhuriwa na Young Lunya, Harmonize, Ibraah, Meneja wa Harmonize, Choppa na wasaniii wengine kibao.

Country Boy  alisainiwa Konde Music Worldwide September 11, mwaka 2020 na kuachia kazi kadha ikiwemo EP yake “The Father EP” lakini pia hits kibao kama Baby, Say, BABA na nyingine nyingi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke