Staa wa Muziki wa Bongofleva Harmonize ameamua kuwajibu wanaomkosoa baada ya Kuonekana akiwa ametoboa pua na kuweka kipini puani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmonize amesema hafanyi hivyo kwa ajili ya kufanana na Wamarekani Weusi , Bali kuwakilisha Tamaduni za Kabila lake la Makonde.
Hatua ya Harmonize kutoboa pua’ yake inakuja siku chache baada ya kuonekana akiwa amevalia sketi jambo liloteka mazungumzo mtandaoni.
Wanamuziki wengine waliowahi kutoboa pua na kuvaa kipini nchini Tanzania ni pamoja na Diamond, Damian Sol na Chidi Beenz.